Askari Wanne Mbaroni Kwa Kusafirisha Wahamiaji haramu

 

Askari Wanne Mbaroni Kwa Kusafirisha Wahamiaji haramu

Jeshi la Polisi Nchini Kenya, linawashikilia Askari wake wanne baada ya Maafisa wa upelelezi kutekeleza oparesheni kwenye nyumba iliyopo kilomita 16 kutoka mji Mkuu wa Nairobina kuwakuta raia 37 wa Ethiopia wakiwa wamepewa hifadhi.


Askari hao, wanadaiwa kuhusika na biashara ya ulanguzi wa Binadamu huku ikiarifiwa kuwa raia hao walikuwa njiani kuelekea Nchi ya Afrika Kusini, ili kutafuta maisha bora ambapo pia bado msako unaendelea ili kumpata mmiliki wake Nyumba hiyo na washiriki wake wa ulanguzi wa binadamu.


Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji – IOM, imeeleza kuwa mara nyingi Wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wamekuwa wakitumia njia ya Kenya kujaribu kuvuka kuingia Afrika Kusini kinyume cha sheria.


Aidha, taarifa hiyo pia inaeeleza kuwa wahamiaji hao ambao wengi wao ni wanaume kutoka mikoa ya Oromia na SNNP, wanaingia Kenya kupitia mpaka wa Moyale, kabla ya kuelekea Tanzania na hatimaye Afrika Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad