Baleke aliondoka Simba dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 mwaka huu, baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika huku akiwa kinara wa ufungaji kikosini hapo kwenye ligi akitikisa nyavu mara nane.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 22 ametangazwa kikosini hapo leo kwa uhamisho wa mkopo akitokea TP Mazembe ambayo kabla ya kumpeleka Al-Ittihad alikuwa Simba kwa mkopo.
Mabao manane aliyoyafunga Baleke kwenye mechi sita yametosha kwa msimu huu na sasa amewaachia nafasi wachezaji wengine wa Ligi Kuu, kuwania kiatu cha ufungaji bora wakiwemo Stephane Aziz Ki wa Yanga anayeongoza mbio hizo akiwa na mabao 10 na Feisal Salumu 'Fei Toto' wa Azam mwenye mabao manane.
Baleke ni miongoni mwa wachezaji sita, walioondoka Simba kwenye dirisha dogo la usajili. Wengine ni Moses Phiri, Jimmyson Mwanuke, Nassor Kapama, Mohamed Mussa na Shaban Chilunda huku ikisajili, Pa Omar Jobe, Freddy Michael, Ladack Chasambi, Babacar Sarr, Edwin Balua na Saleh Karabaka.