Bashungwa awasili Morogoro, atekeleza agizo la Rais Samia kufika pasipofikika

 

Bashungwa

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema dhamira ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona Watendaji wa Wizara ya Ujenzi wanafika katika maeneo yasiyofikika kutatua changamoto za miundombinu ya barabara na madaraja nchini.


Waziri Bashungwa ameeleza hayo Mkoani Morogoro wakati alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku nne na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima, leo tarehe 21 Februari 2024.


“Mheshimiwa Rais anataka kuona mimi na Watendaji wangu tunafika sehemu zisizofikika, ikiwa ni pamoja na maeneo ya vijijini ambako kuna mitandao ya barabara za TANROADS, tumekuja kutekeleza maelekezo hayo, tutahakikisha tunafika kwa kutembea kwa miguu, kupanda mitumbwi hata kutumia bodaboda, kutatua changamoto za miundombinu ya barabara na madaraja” amesema Bashungwa.


Waziri Bashungwa amesema Morogoro ni mkoa wa kimkakati katika kilimo na shughuli mbalimbali za uzalishaji ambao unahitaji miundombinu bora ili kuhakikisha shughuli zinafanyika kwa ufanisi.


“Tunaona jitihada za Serikali katika mkoa huu za ujenzi wa miundombinu ikiwani Pamoja na reli ya SGR ambayo ulipo mbioni kuanza, kuanzia Dar es salaam kupita Morogoro Mpaka Dodoma, hata sisi Wizara ya Ujenzi tuna mpango wa kujenga barabara kutoka Kibaha kupita Morogoro hadi Dodoma ili kurahisisha shughuli za kiuchumi”, amesisitiza Bashungwa.


Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema ziara hiyo ina manufaa kwa mkoa wa Morogoro ambao ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika na mvua za El Nino ambapo sasa Waziri Bashungwa atajionea athari hizo na kupata ufumbuzi wa kurejesha miundombinu hiyo pamoja na miradi inayoendelea kutekelezwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad