Beki Inonga Afanya Maamuzi Kimya Kimya, Asign Mkatabata wa Awali



Kwa kiswahili cha kijiweni wanasema; “Imeisha.” Beki kitasa cha Simba aliyeng’ara na DR Congo kwenye Afcon, amefanya uamuzi wake kimyakimya na akapiga kimya vilevile. Na uamuzi huo unamaanisha kwamba atakuwa ndani ya jezi ya Simba katika mechi zisizozidi 15 tu za mzunguko wa pili wa ligi, baada ya hapo ndiyo hivyo tena.
.
Habari za uhakika kabisa kutoka kwenye vyanzo ni kwamba staa huyo ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu, amesaini mkataba wa awali na FAR Rabat inayoongoza Ligi Morocco.

Kumbuka hii ndiyo timu anayoichezea Bernard Morrison ikifundishwa na Kocha wa zamani wa Yanga, Nabi Mohammed. Inonga tayari amerejea nchini akitokea kwao DR Congo baada ya kuiwezesha nchi yake kuwa mshindi wa nne katika AFCON. Taarifa kutoka nchini Morocco ni kwamba Inonga ameingia makubaliano ya awali na klabu ya FAR Rabat ambayo yatamfanya mwisho wa msimu kwenda kusaini mkataba wa miaka mitatu na vinara hao wa Ligi ya nchini humo maarufu kama Botola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad