Belouizdad Haikuwa 'Level' ya Yanga

Belouizdad Haikuwa 'Level' ya Yanga


Yanga haijapoa. Bado inafurahia ushindi wa mabao 4-0 ilioupata wikiendi iliyopita dhidi ya CR Belouizdad ya Morocco katika mechi ya kundi D la hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na tunaendelea inaendelea kukupa 'fact' za mechi hiyo na leo inakupa hii kuhusu timu za taifa.


Katika mechi hiyo ambayo iliiwezesha Yanga kwa mara ya kwanza katika historia yake kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kikosi chake kiliiacha kwa mbali Belouizdad kwenye viwango (levo) za wachezaji na timu za taifa.


Miongoni mwa mafanikio wanayojivunia zaidi wachezaji duniani kote ni kucheza kwa mafanikio katika timu zao na ya timu za taifa, na kwa Afrika ni kushiriki michuano mikubwa kama fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambazo kwa msimu huu zilifanyika nchini Ivory Coast, ambako wenyeji walitwaa taji hilo katika michuano iliyomalizika Februari, mwaka huu.


Hapo ndipo Yanga inaipiga gepu tena Belouizdad kwani wachezaji saba waliocheza mechi hiyo walikuwa kwenye Afcon msimu huu na timu za mataifa mbalimbali, huku Belouizdad kikosi chake kikiwa hakina hata nyota mmoja aliyeshiriki Afcon.


Kwa Yanga nyota waliokipiga Afcon ni kipa Djigui Diarra; mabeki Dickson Job, Ibrahim Abdallah 'Bacca', Bakari Mwamnyeto ilhali viungo kuna Mudathir Yahya, Stephane Aziz Ki na upande wa ushambuliaji yupo Kennedy Musonda.


Jumamosi iliyopita, wachezaji hao walicheza dhidi ya Belouizdad kasoro nahodha, Mwamnyeto.


Job, Bacca, Mwamnyeto na Mudathir walikuwa na timu ya taifa ya Tanzania iliyotolewa hatua ya makundi sawa na Zambia aliyokuwa akiichezea Musonda.


Aziz Ki alikuwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichotolewa na Mali katika hatua ya 16 bora, huku Diarra akiwa na Mali iliyoondoshwa katika robo fainali kwa kufungwa mabao 2-1 na mabingwa Ivory Coast.


Jambo la kufurahisha zaidi kwa wababe wa Jangwani ni kwamba, nyota wake watatu waliokuwa Afcon yaani Mudathir, Aziz Ki na Musonda kila mmoja alifunga bao dhidi ya Belouizdad kasoro Joseph Guede ambaye ni staa mpya kikosini na hakuwepo Afcon.


Wachezaji wengi waliounda kikosi cha Belouizdad ni raia wa Algeria, taifa ambalo katika Afcon msimu huu liliburuza mkia katika kundi D, huku Angola na Burkina Faso yakitinga hatua ya 16 bora kutoka kundi hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad