BREAKING: Waziri Nape Aruhusu Magazeti Kusoma Kwa Mbwembwe na Ubunifu Baada ya Jana Kukatazwa na TCRA



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema kuwa ameruhusu waandishi wa habari kusoma magazeti kwa ubunifu.

“”Nimeona mjadala wa “kusoma magazeti”. Nimeelekeza TCRA kuruhusu UBUNIFU kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza MVUTO kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa KUTIWA MOYO badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti.”” - amesema @napennauye

Hii inakuja baada ya Mhandisi Andrew Kisaka, Mkuu wa Kitengo cha leseni TCRA, kusema kuwa waandishi wa habari wanaoongeza mbwembwe kwenye usomaji wa magazeti watachukuliwa hatua.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad