Azimio hilo la Bunge limesomwa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada ya muongozo wa Spika ulioombwa na George Mwenisongole Mbunge wa Jimbo la Mbozi kuhusu matangazo ya nafasi za kazi yanayotolewa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vyombo vingine vya Serikali ambavyo vinataka Muombaji awe amepitia mafunzo ya JKT akidai kuwa kigezo hichi kinawaondoa ambao hawajapata fursa ya kupita kwenye mafunzo hayo.
Akisoma azimip hilo Dkt. Tulia amesema “kwakuwa Jeshi la Kujenga Taifa JKT na Jeshi la Kujenga Uchumi JKU hayana uwezo wa kumudu na kupokea na kuwafundisha Vijana wote wanaohitimu kidato cha nne na cha sita na kuwa upo uwezekano wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwapeleka JKT na JKU Vijana watakaokuwa wameajiriwa kwa kukidhi masharti ya msingi ya ajira husika na kwakuwa wapo Vijana wenye sifa na uwezo na wanaweza kutimiza masharti ya ajira kwenye Vyombo vya Ulinzi isipokuwa sharti la kupitia JKT na JKU Bunge linaazimia Vijaa wote wapewe fursa sawa kwenye ajira pale wanapokuwa wametimiza masharti yanayohusuka na ajira husika”