CAF Waijaza Taifa Stars Mijihela Kisa Mashindano ya AFCON


Licha ya kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023), timu ya taifa 'Taifa Stars' imefanikiwa kupata Sh1.2 bilioni baada ya kumaliza hatua ya makundi ya fainali za Afcon 2023 ikiwa nafasi ya nne.

Stars ambayo haikupata ushindi kwenye kundi F ambapo ilikuwa na Morocco, DR Congo na Zambia iliambulia sare mbili dhidi ya DR Congo na Zambia.

Kiasi hicho cha fedha ni zawadi inayopata timu ya mwisho kwenye kundi kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) huku timu zilizomaliza nafasi ya tatu zikipata Sh1.7 bilioni na zilizofuzu hatua ya 16 bora zikivuta bilioni 2.

Stars ilikusanya pointi mbili kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia na ya bila kufungana mbele ya DR Congo ambayo ilicheza nayo mechi ya mwisho ya kundi F.

Katika mashindano ya mwaka huu CAF imeongeza zawadi ambapo mshindi atapata zaidi ya Sh16 bilioni ikiwa ni ongezeko la Sh4.7 bilioni kutoka Sh12 bilioni ambazo ilizipata Senegal kwa kuibuka bingwa kwenye fainali zilizopita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad