DC Aagiza Kufungwa kwa Taasisi ya Mango Kinder Bagamoyo

 

DC Aagiza Kufungwa kwa Taasisi ya Mango Kinder Bagamoyo

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash (@okash_halima ) ameagiza kufungwa kwa Taasisi ya Mango Kinder iliyopo Kata ya Dunda Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya kituo hicho kukiuka utaratibu wa leseni yake ya kutoa haki kwa Watoto na badala yake kuwakusanya Watoto zaidi ya 200 na kuwapa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo yaliyo kinyume na maadili ya Mtanzania chini ya ufadhili wa Raia wa Ujerumani.


Kituo hicho huwakusanya Wanafunzi kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni na kuwapikia chakula kisha kuwafundisha masuala mbalimbali bila ya kibali ambapo DC Halima ameagiza pia kusitishwa kwa kibali cha Taasisi hiyo na leseni na ameitaka Kamati ya Usalama kuondoka na Mmiliki wa Taasisi hiyo Mtanzania Franky Silvester Neumann na Timu yake akiwemo Mke wa Franky ambaye ni Raia wa Ujerumani ili wakahojiwe zaidi.


Awali wakati wa mahojiani yake na DC, Franky amesema “Mimi nilikuwa Ujerumani nikawaambia Tanzania nina Watoto hali yao sio nzuri, wakanipa ufadhili Euro 1000 kila mwezi tuwe tunawapikia Watoto chakula, wakimaliza wanasoma msomo mbalimbali”


DC Halima amesema “Tumekuta zana mbalimbali ambazo inatupeleka kugundua Watoto hawafundishwi maadili mema na mengi ya mambo wanayofundishwa ni mambo ya kijinsia ambayo yanakiuka taratibu na mila na desturi zetu”


“Nimeelekeza tutasitisha kibali na leseni ya Taasisi hii na wote wanaohusika na Taasisi tutaondoka nao kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi lakini hili eneo halitotumika tena, hawa Watoto tangu November mwaka jana wanakuja hapa na Watu hawatoi taarifa kwa wakati, utamaduni wa kwetu wanaenda kuubadilisha”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad