Diamond Afunguka: Nimebaki Mjane, Naomba Faraja zenu

Diamond Afunguka: Nimebaki Mjane, Naomba Faraja zenu


Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa kwa sasa anahitaji faraja baada ya kubaki mjane kufuatia kupigwa chini na mpenzi wake, Zuchu.


Hii inatokana na Diamond kuposti video akiwa na mama watoto wake, Zari huku akimuita kuwa ni dada yake, jambo ambalo lilimkera Zuchu na kuamua ktangaza kuvunja rasmi mahusiano yake na Mondi.


Muda mfupi baada ya Zuchu kutangaza kuachana rasmi na Diamond Platnumz, hatimaye Chibu Dangote ametoa tamko lake.


"Basi bwana wadau, ndio kama mlivyosikia matikiti yamenidondoke, hivyo nahitaji sana huruma na ukaribu wenu kipindi hiki cha ujane wangu, ili walau kupata nguvu na faraja kwenye kipindi hiki kigumu," amesema Diamond.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad