Edo Kumwembe “Tatizo la Mayele ni Majivuno Fulani Ambayo Anayo"


“Tatizo la Mayele ni majivuno fulani ambayo anayo. Anafahamu kauli yake itazua taharuki nchini kwa sababu bado ni maarufu hapa nchini. Angeweza kukaa kimya tu na kufanya mipango yake kuliko kujali sana masuala ya mitandao ya kijamii. Haimsaidii.
.
Wachezaji wa kulipwa kazi yao ni kucheza soka na kupuuza kelele za mashabiki. Mashabiki kazi yao kubwa pia ni kukutoa mchezoni. Kukabiliana na changamoto za wachezaji wa timu pinzani, pia mashabiki wa timu pinzani pamoja na wale mashabiki wako ni kazi ya mwanasoka wa kulipwa.
.
Kuelekea pambano la Pyramids na Mamelodi pale Afrika Kusini, Mayele alikuwa amenyimwa viza ya kuingia Afrika Kusini. Akaenda katika mtandao wake na kuandika kwamba huo ulikuwa mpango tu wa Mamelodi kuhakikisha hachezi pambano hilo. Kocha wa Mamelodi, Rhulani Mokwena akamjibu Mayele aachane na mambo ya mitandao.”

- Edo Kumwembe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad