Goli la Mudahir Yaiweka Yanga Kileleni, Simba na Azam Wanakazi ya Kufanya



WE Mudathir umepigaje hapo? Ndivyo mashabiki wa Yanga walivyokuwa wakijiuliza kwa furaha baada ya kiungo huyo mzawa na mzoefu wa Chamazi, kuifungia timu yake bao la ‘jioooni’ kabisa katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Azam Complex na kuwapandisha mabingwa hao kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Mudathir aliyeingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude aliifungia Yanga bao hilo dakika ya 86 akiunganisha krosi ya mtokea benchi mwenzie Nickson Kibabage aliyepokea pasi nzuri ya Pacome Zouzoua ambaye kwanza aliwachekecha mabeki.

Bao hilo muhimu lilitosha kuirudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikifikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 13 na kuishusha Azam hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 31 zote zikicheza mechi 13,

Mahasimu wao Simba, ambao wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 26, watacheza mechi yao ya 12 ya Ligi Kuu leo dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi leo.
Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata ushindi huo katika mechi ambayo wageni, Dodoma Jiji walicheza vyema bila ya wachezaji kutumia mbinu zilizokithiri za kupoteza muda kama walivyocheza Kagera Sugar katika mechi nyingine ya kiporo ya Yanga iliyochezwa Ijumaa kule Kagera,

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi kabla ya maechi yao ya jana, aliitaka Dodoma Jiji icheze mpira wa kuvutia kwa ajili ya mashabiki wao, isiwe kama Kagera Sugar ambayo ilikuwa ikipoteza muda, na walima zabibu hao wakacheza kama alivyotaka, lakini Wanajangwani hawakuwa na maajabu kwa muda mwingi wa mchezo.

Licha ya Jiji kutopaki basi, Yanga ilipata wakati mgumu kuipenya ngome hiyo huku mshambuliaji mpya Joseph Guede, akionekana bado anahitaji muda mwingi wa kuwa fiti zaidi.
Pacome aliendelea kuwa mtu muhimu katika kikosi hicho akicheza vyema pamoja Khalid Aucho, lakini Maxi Nzengeli alionekana kupania zaidi kufunga ili kumaliza ukame wa mabao unaomkabili kwenye Ligi Kuu Bara na hivyo kujikuta akipoteza nafasi kwa kujaribu kufunga mwenyewe,

Dodoma Jiji walichofanikiwa kwenye mchezo huo ni kuzuia mashambulizi huku wakimuacha Mshery hana kazi ya kufanya kutokana na kushindwa kupeleka mashambulizi kwa wapinzani wao,

Mechi iliendeleza rekodi mbaya ya Dodoma Jiji dhidi ya mabngwa hao kwani sasa katika mechi saba walizokutana tangu walipopanda daraja mwaka 2020 wamepoteza sita kwa juma la mabao 15-3, huku wakiambulia sare moja tu ya bila kufungana Julai 18, 2020.


GIFT AMTISHA MWAMNYETO
Beki wa kimataifa wa Uganda na Yanga, Gift Fred alicheza kwa kiwango bora tangu alipo aminiwa katika mashindano ya Mapinduzi mpaka kwenye hizi mechi za mbili za Ligi Kuu Bara.
Gift akishirikiana na Job alionekana kuepuka kufanya makosa binafsi jambo ambalo linaweza kumpa presha nahodha Bakar Mwamnyeto.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad