Taylor Swift alitawala maonyesho ya Tuzo za Grammy za mwaka huu, kwa kuwa mwigizaji wa kwanza kushinda tuzo ya albamu ya mwaka mara nne.
Nyota huyo hapo awali alikuwa ameshinda tuzo tatu za albamu bora akiwa na Stevie Wonder, Paul Simon na Frank Sinatra.
Alipokea tuzo kutoka kwa Celine Dion, ambaye alionekana kwa kushtukiza . Swift pia alitumia tukio hilo kufichua albamu yake mpya iliowashangaza wengi.
Miley Cyrus na Billie Eilish walitwaa tuzo nyingine bora katika sherehe za Jumapili.
Mchango wa Eilish kwenye wimbo wa filamu ya Barbie, What Was I Made For?, ulishinda wimbo bora wa mwaka, akiishinda Anti-Hero ya Swift pamoja na nyimbo za SZA, Cyrus na Olivia Rodrigo.
"Kila mtu katika kitengo hiki - ilikuwa orodha ya watu wenye vipawa vya ajabu, wasanii wa ajabu, muziki wa ajabu. Nasikia furaha sasa hivi."
Wimbo huo pia ulishinda wimbo bora zaidi ulioandikwa kwa vyombo vya Habari vinavyotumia video, huku albamu ya Barbie - ambayo iliwekwa pamoja na mtayarishaji Mark Ronson - iikishinda tuzo ya wimbo bora wa mkusanyo wa vyombo vya habari vya kuona.