Gwajima: Daktari alifanya upasuaji Zanzibar akiwa Dar

Gwajima: Daktari alifanya upasuaji Zanzibar akiwa Dar


Mbunge wa Jimbo la Kawe, Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima amehoji juu ya maandalizi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya akili mnembe [Artificial Intelligence] ambayo inaonekana kupoteza ajira za watu wengine.


Amesema Januari 27, 2024 yalifanyika majaribio ya mwalimu kufundisha Dodoma akiwa Kibaha – Pwani na jaribio jingine ambalo daktari alifanya upasuaji Zanzibar akiwa Dar es Salaam na upasuaji huo ukafanikiwa.


Amehoji pia kutokana na matumizi mengine kama ya roboti kufanya shughuli za binadamu, Serikali imejiandaa vipi na upotevu wa ajira kutokana na teknolojia hizo kuchukua ajira za Wananchi.


Hayo yamejiri Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa Bunge unaoendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad