Henock Inonga na Chama Wakosekana Kwenye Kikosi cha Simba Kuelekea Kigoma, Kocha Benchika Anena

 

Henock Inonga na Chama Wakosekana Kwenye Kikosi cha Simba Kuelekea Kigoma, Kocha Benchika Anena
Kocha Benchika na Chama

Henock Inonga na Chama Wakosekana Kwenye Kikosi cha Simba Kuelekea Kigoma, Kocha Benchika Anena

Simba imeondoka asubuhi hii ikienda Kigoma kuifuata Mashujaa FC, lakini katika safari hiyo kiungo Clatous Chama amekosekana.


Katika msafara wa Simba ambao umeondoka Dar es Salaam wamekosekana mastaa wawili pekee akiwamo Chama ambaye awali alikuwa alisimamishwa pamoja na beki Henock Inonga aliyepo kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zinazoendelea nchini Ivory akiwa na timu ya Taifa ya DR Congo.


Kocha Abdelhak Benchikha amezungumzia kwa kifupi juu ya Chama akisema hajajiunga na timu na wala hajui atajiunga lini.


"Chama? Bado hajajiunga na timu. Hawa ndio wachezaji tunaondoka nao kwenda kucheza mechi mbili ngumu za ugenini," amesema Benchikha.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema Chama tayari ameshatua nchini huku alitarajiwa kusafiri wakati wowote kuanzia kesho kuungana na wenzake.


Benchikha ameendelea kusisitiza ratiba ya mechi ni ngumu ambapo hajajua wanakwenda kukutana na aina gani ya viwanja.


"Hizi ni mechi zilizo karibu sana. Nimewaambia wachezaji wajiandae kiakili. Hatujajua tutakwenda kukutana na viwanja vyenye ubora wa aina gani, lakini tunatakiwa kwenda kupambana na mazingira yoyote tutakayokutana nayo huko," amesema.


Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23, huku Mashujaa FC ikiwa nazo tisa ikiwa katika nafasi ya 15.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad