Huitaji Degree Kujua Kama Brand ya Yanga Imekua Sana Kwa Sasa

 

Huitaji Degree Kujua Kama Brand ya Yanga Imekua Sana Kwa Sasa

Huko nyuma brand ya yanga ilishuka sana hasa baada ya Yusuph manji kuondoka.


Wakati brand ya yanga ikishuka ndio wakati brand ya Simba ilikuwa inapanda baada ya Mo Dewji kuingia mitaa ya msimbazi.


Kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 simba ilifanikiwa kujitambulisha katika soka la Afrika.


kuanzia 2022 hadi sasa ni kama Kuna mahali wamejikwaa kidogo. Ukiangalia wanaendelea kuishi katika historia ya 2019 - 2022, Kimsingi grafu yao inapanda kwa kusua sua.


2022 Hadi sasa wananchi wameimarika sana, timu yao imetawala soka la ndani na wajitambulisha hadi katika soka la Afrika.

By Hekima Kibona


Chini ya uongozi wa hersi said na mfadhili wa klabu [GSM], wameipeleka brand ya yanga katika level nyingine.


Wawekezaji na makampuni mengi kwa Sasa yanitazama yanga kama sehemu sahihi kwenda kuweka pesa zao.


Kiukweli sio rahisi kujenga brand hadi ukakubalika na watu, inahitaji akili na kufanya vitu vya ziada ambavyo pengine havofanywi na wengine.


Imani yangu ni kuendelea kuona klabu zetu zikiendelea kukukua zaidi na zaidi ili soka letu liendelee kuwa na ushindani.


NB: nikisema niwaulize hapa kati ya Simba na yanga kwa Sasa timu ipi brand yake ipo juu? Mtanipa majibu mchanganyiko. Kwa kutumia tu akili ya kawaida unaelewa kuwa brand ya yanga imepanda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad