Kocha Benchikha Akasirika na Mastaa Simba

Kocha Benchikha Akasirika na Mastaa Simba


Juzi Simba imeshinda bao 1-0, dhidi ya Mashujaa, Kigoma na kesho itajitupa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kucheza na Tabora United ikiwa ni muendelezo wa viporo vyake katika Ligi Kuu huku kocha mkuu wa chama hilo, Abdelhak Benchikha akiendelea kukomaa viwango wanavyoonyesha mastaa wake.


Ushindi huo mwembamba uliopatikana kwa bao la mkwaju wa penalti lililofungwa na Saidi Ntibanzokiza uliifanya Simba kufikisha alama 26 katika nafasi ya tatu kwneye msimamo baada ya mechi 11, nyuma ya vinara Azam wenye pointi 31 baada ya mechi 13 na nafasi ya pili ipo Yanga na alama 31 baada ya mechi 12.


Taarifa kutoka kambi ya Simba zinaeleza kocha huyo hakuridhishwa na ubora waliouonyesha baadhi ya wachezaji katika mechi na Mashujaa na kuwataka wabadilike haraka.


Benchikha aliwaeleza wachezaji wanakabiliwa na mechi ngumu mfululizo hivyo wanatakiwa kujitoa zaidi kwaajili ya timu ili kuhakikusha wanapata ushindi na kupunguza presha.


"Kama kawaida baada ya mechi tulikuwa na kikao. Kocha alitupongeza kwa ushindi lakini aling'aka kwa kiwango cha timu kwa ujumla. Hakufurahia namna tulicheza," kilisema chanzo hicho ambacho ni kati ya wachezaji wa timu hiyo aliyeongeza;


"Ukiachana na timu, kuna wachezaji mmoja mmoja aliwachana mbele yetu na kuwaambia wanahitaji kubadilika haraka na mabadiliko hayo ayaone kwenye mechi mbili zijazo."


Mchezo wa kesho utakuwa wa 12 kwa Simba kwenye ligi msimu huu na kama itashinda itafikisha alama 29 na kusalia nafasi ya tatu na baada ya mechi hiyo itasafiri hadi jijini Mwanza kwa ajili ya mechi mbili za ligi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, ikianza na Azam Februari 9 kisha kumalizana na Geita Gold, Februari 12.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad