Kocha Gamondi Akuna Kichwa na Kuamua Kubadili Gia Angani Kisa Uhaba wa Magoli

Kocha Gamondi Akuna Kichwa na Kuamua Kubadili Gia Angani Kisa Uhaba wa Magoli


Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema baada ya kuambulia pointi nne kwenye mechi mbili za ligi zilizochezwa hivi karibuni anatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kwa kuwa ratiba inawabana.


Yanga imekusanya pointi hizo baada ya suluhu dhidi ya Kagera Sugar ugenini na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji juzi kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi aliwapongeza wachezaji wake kwa kutokukata tamaa licha ya kutengeneza nafasi nyingi dhidi ya Dodoma na kushindwa kuzitumia na kuendelea kupambana hadi dakika za mwisho wa mchezo hali iliyowafanya waibuke na ushindi huo mwembamba.


"Wachezaji wangu wamecheza vizuri, kukosa nafasi ni sehemu ya mchezo jambo zuri ni kwa kuwa hawajakata tamaa, wamepambana na kunipa pointi tatu, hilo limeongeza morali na naamini katika michezo ijazo watacheza kwa kujiachia bila presha.


"Pia kutokana na ugumu wa ratiba natarajia kufanya mabadiliko makubwa ya mara kwa mara kwenye kikosi ili kutoa nafasi ya wachezaji wengine kukusanya nguvu mpya huku wengine wakipambania timu kufikia malengo." alisema.


Gamondi alisema wachezaji wake hawana muda wa kupumzika na wamekuwa na mechi mfululizo hivyo ili kutafuta usawa analazimika kumtumia kila mchezaji ili kutoa mapumziko kwa wengine.


"Tumecheza leo, siku mbili mbele tuna mchezo mwingine wachezaji wanakosa muda wa kurudisha utimamu wa mwili, hilo linaweza kuwasababishia majeraha madogo madogo, ili kuepuka hayo nitafanya mabadiliko ya mara kwa mara na wala mtu asishangae.


"Nina imani kubwa na wachezaji waliopo kikosini, naamini kila mmoja atafanya kazi yake kwa usahihi akipata nafasi ya kucheza, lengo ni moja kukusanya pointi zitakazotufanya tuweze kutetea ubingwa msimu huu," alisema kocha huyo raia wa Argentina.


Akizungumzia matokeo waliyo yapata dhidi ya Dodoma Jiji, Gamondi alisema bao walilofunga litasaidia kupunguza presha kwa wachezaji na anaamini mechi zijazo watacheza kwa kujiamini zaidi na kutumia nafasi.


"Timu ilikuwa inacheza kwa presha kila mchezaji alikuwa anatamani kufunga lakini haikuwa rahisi hivyo naamini ushindi wa bao moja dhidi ya Dodoma Jiji utaamsha hali ya ushindani na mwendelezo mzuri wa kufunga." alisema.


MECHI ZA YANGA


Yanga vs Mashujaa Februari 8


Tanzania Prisons vs Yanga Februari 11


KMC vs Yanga Februari 17


JKT Tanzania vs Yanga Februari 25

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad