Nilivyoona tu taarifa za kocha Adel Amrouche kuwapokea Cr Belouizdad, akili yangu ikakumbuka nyuma kidogo...
Nimekumbuka kipindi kile Haji manara wakati yupo Simba alivyotuhumiwa kuuza mechi ya derby dhidi ya yanga, kwa ushahidi kuwa alionekana na viongozi wa yanga hotelini.
Akili yangu ikanipeleka hadi Ivory coast katika #AFCON23 nikakumbuka Legend wa nchi hiyo alivyokuwa karibu na baadhi ya wachezaji wa mataifa mengine hasa Victor Osimhen wa Nigeria. Lakini hakuna pahala alituhumiwa kuhujumu taifa lake.
Nikakumbuka pia kipindi ambacho simba walikuwa wanakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika kusini katika michuano ya klabu bingwa.
Simba walimtuhumu sana Injinia Hersi ambaye ni Rais wa yanga kwa sasa kwa kuwa na ukaribu na viongozi wa kaizer chiefs hadi jezi zao akawa anavaa.
Mwishoni yeye mwenyewe alifafanua kuwa kaizer ni ndugu zao na jezi yao huwa anavaa siku ambayo tuko na FURAHA.
Tuchane na huko. Kocha Adel Amrouche ni raia wa Algeria na Cr Belouizdad ni klabu kutoka Algeria.
Ni kweli anaweza kuwauzia mbinu Belouizdad? Inawezekana, lakini nawaza angetaka kuwauzia, hiyo ndio njia pekee? Hapana angeweza hata kuwasiliana nao kwa simu na akawauzia.
Guys, iko wapi fair play katika soka? Tunataka wageni kupokelewa iwe jinai? Bila shaka hapana, hapa @tanfootball sidhani kama wana haja ya kuhangaika.
Wananchi waendelee kuandaa timu yenye ushindani. Hizi propaganda zisiwatoe kwenye reli.
✍️ @hekimakibona_