Maisha Yatakuwa Magumu Sana Kwa Simba Endapo Watafungwa na ASEC Mimosas




ASEC MIMOSAS V/s SIMBA ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili, lakini ni muhimu zaidi kwa Simba kwa sababu bado haijafuzu hatua ya Robo Fainali, ASEC Mimosas yenyewe tayari imejihakikishia kucheza Robo Fainali.

Katika mchezo huu Simba inahitaji alama tatu au alama moja, endapo itapata alama tatu itafikisha alama nane na ikiwa itashinda mchezo wa mwisho nyumbani [Benjamin Mkapa Stadium] dhidi ya Jwaneng Galaxy itakuwa imefuzu Robo Fainali.

Ikitokea leo Simba ikapata alama moja itafikisha alama sita, kama itashinda mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy itafikisha alama tisa. Alama hizo zinaweza kufikiwa na Wydad kama itashinda mechi zake mbili dhidi ya Jwaneng Galaxy na ASEC Mimosas.

Kama Simba na Wydad zitalingana alama, Simba ina faida ya kushinda kwa idadi kubwa ya magoli katika mechi mbili ambazo timu hizo zilikutana. Simba ilipoteza 1-0 dhidi ya Wydad ugenini lakini ikashinda 2-0 nyumbani.

Kama Simba itapoteza leo dhidi ya ASEC Mimosas halafu Wydad ikashinda dhidi ya Jeaneng Galaxy, Simba itakuwa kwenye wakati mgumu sana wa kufuzu kwa sababu hata ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha alama nane na Wydad ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha alama tisa.

Kwa hiyo ili Simba iendelee kubaki na matumaini makubwa ya kwenda hatua ya Robo Fainali inapaswa kupata alama tatu au moja kwenye mchezo wa leo dhidi ya ASEC Mimosas.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad