Idara ya Uhamiaji inawatangazia vijana waliotuma maombi ya nafasi ya Ajira kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kufika kwenye usaili utakaofanyika katika Ukumbi wa Auditorium - CIVE uliopo Ndaki ya Sayansi ya Kompyuta na Elimu Angavu katika
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) siku ya Jumamosi ya tarehe 24 Februari, 2024 saa 1:00 kamili asubuhi.
Kwa wale waliotuma maombi kupitia Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kufika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja siku ya Jumamosi tarehe 24 Februari, 2024 saa 1:00 asubuhi.
Waombaji wote wanatakiwa kufika na Vyeti Halisi (Original Certificates); Cheti cha Kuzaliwa, Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Vyeti vya Taaluma, Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kutoka JKT/JKU, Vyeti vingine vya Uhitimu wa mafunzo katika fani mbalimbali na Kalamu ya wino ya buluu.
Waombaji ambao Muundo wa fani zao unatakiwa kusajiliwa na Bodi za Taaluma, wanatakiwa kufika na Vyeti vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi katika fani husika.
WAOMBAJI AMBAO HAWATAFIKA NA VYETI HALISI, HAWATARUHUSIWA KUFANYA USAILI.
Aidha, wasailiwa wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi husika.
Tahadhari:
Mwombaji yeyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.
READ FULL DETAILS THROUGH THE PDF DOCUMENT BELOW:
About Immigration Tanzania
The Tanzania Immigration Services Department (Immigration Tanzania) is established under Section 4(1) of the Immigration Act of 1995 Chapter 54 as amended by Act No.8 of 2015. It gives the Department the authority to control and facilitate immigration issues in the United Republic of Tanzania. The Department is one of the security organs under Ministry of Home Affairs. To become an efficient and effective Institution, which provides high quality Immigration services that meet both national and international standards. To facilitate and control movements of persons through implementation of relevant Laws and Regulations in order to safeguard national security and economic interests. Passport is one of the very sensitive document issued by the government to its citizens so as to allow them to travel outside the country for various purposes. Tanzania government issues various types of passports and other travel documents as provided for by the Tanzania Passports and other Travel documents Cap 42 of 2002 and its Regulations of 2004. The passport pages for the current electronic passport contains various images and drawings which explicates the country’s history and tourist attractions.