MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) Yatabiri Mvua Kubwa



MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imesema mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mikoa ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

TMA imeeleza mvua za nje ya msimu zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kuungana na mvua za Masika 2024 na zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2024.

Hayo yameelezwa leo Februari 22, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Ladislaus chan’ga alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu wa masika.

Aidha, Dk Chan’ga amesema ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia, Dar es salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba unatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani mapema wiki nne ya Mwezi Februari 2024 na kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024.

Pia, Dk Chan’ga amesema Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi (Pwani ya Afrika Mashariki) ikilinganishwa na upande wa mashariki mwa Bahari ya Hindi. Vilevile, joto la bahari la chini kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la Kusini mwa kisiwa cha Madagascar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad