Manara Aibuka Kuwatetea Wamasai kupigwa marufuku Wasitembee na Silaa Zanzibar

Manara Aibuka Kuwatetea Wamasai kupigwa marufuku Wasitembee na Silaa Zanzibar


Manara aibuka kuwatetea Wamasai baada ya kupigwa marufuku wasitembee na rungu wala sime Zanzibar

"Nikiwa kama Morani Mkuu wa huku Social Media nimeona niseme kitu na nitoe ushauri wangu kuhusu sakata la bakora zetu za juzi ( Siungi mkono violence )

Kiasili Sisi Wamasai sio Watu wagomvi na hatupendi shari hata kidogo, lakini tuna shida kubwa moja, hatupendi kunyanyaswa wala kuonewa hata kidogo, hatuna udhaifu katika kutetea haki zetu, TUKICHOKOZWA TUNACHOKOZEKA.

Tumeona pia katazo la kutembea na silaha zetu za jadi kwa dhana ya kulinda utamaduni wa Zanzibar, ifahamike kabila letu ni miongoni mwa makabila machache yaliyobaki duniani, ambayo yanadumisha utamaduni na mila zake, kutuzuia kwa sababu yoyote ile ni kutunyanyasa kisaikolojia!! Tunahofia mtakuja kutuzuia hata kutembea bila boxer wakati sio mambo yetu!!

Vipi hamzuii Walami wanaotembea nusu utupu kwenye mitaa ,mje mtuzuie Watanzania wenzenu? Kutembea utupu kwa Watasha ni utamaduni wa Zanzibar? Lakini utawakatazaje wakati kwao sio dhambi, iweje mtuzuie sisi Waafrika wenzenu.

Viongozi wangu nawaomba chezeni Biti ya Rais Dr Hussein Mwinyi, Biti nzuri ya Uchumi wa Buluu, Biti ambayo Sisi Wamasai tunaoishi Zanzibar tunaicheza kwa midundo yote,tunashiriki kikamilifu katika kuusapoti utalii wetu, msitufanyie hivyo tukaja kujihisi manyanyaso !!

Tunaipenda sana Zanzibar na tunaheshimu tamaduni zenu na ndio maana hata Taarabu tunaweza kuimba siku hizi, tunacheza hadi Msewe na kidumbak, tunakula urojo na mikate ya boflo, ilhali sisi chakula chetu kikuu ni Maziwa na Nyama.

Chonde Chonde tuishi kwa kuvumiliana ndugu zangu,,Sisi ni Wamoja na Zanzibar ni second home ya Wamasai 🙏🙏

Bugati

Morani Mkuu El Mundo 🔥"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad