Mgonjwa Afariki Dunia kwa Kujinyonga Akiwa Wodini

 

Mgonjwa Afariki Dunia kwa Kujinyonga Akiwa Wodini

Batromeo Bernad, Mkazi wa Mtaa wa Ndege Wengi, uliopo mkoani Morogoro, amefariki dunia kwa kujinyonga na shuka akiwa wodini katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.


ITV imezungumza na baadhi ya ndugu wa marehemu, ambao wamedai kuwa walimfikisha Batromeo Hospitali hapo, wiki mbili zilizopita, akisumbuliwa tatizo la afya ya akili, ambapo wameomba utaratibu wa ndugu mmoja kuruhusiwa kubaki na mgonjwa hospitalini hapo.


Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, ITV imezungumza na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha bado wanaendelea na uchunguzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad