Mlipuko Mkubwa Waua Watu Kadhaa na Kujeruhi Kenya



Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika kijiji cha Mradi, mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi baada ya mtambo wa gesi kulipuka muda mfupi kabla ya sita usiku wa Alhamisi, na kuliingiza jiji katika hofu, gazeti la Daily Nation liliripoti.

Wengine dazeni kadhaa wanaripotiwa kupata majeraha ya kutishia maisha.

Takriban saa mbili baada ya milipuko kadhaa iliyopelekea moto na moshi kutanda angani, huduma za dharura, wakiwemo wazima moto, walikuwa bado hawajafika katika eneo la tukio, kulingana na mashahidi.

"Milipuko mikubwa ilisikika, huku watu wakipiga kelele na kukimbia kila mahali kwa kuhofia milipuko zaidi,” mtu mmoja aliyeshuhudia aliliambia gazeti hilo.

Moto huo umeteketeza majengo jirani, huku wakazi wa makazi jirani kama vile Nyayo Embakasi wakitoka kwa wingi huku wakipiga mayoe kwa hofu.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura aithibitisha kisa hicho na kusema kwamba mlipuko huo ulitoka kwa kiwanda cha gesi kilichokuwa katika enel la makazi.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na kikosi cha zima moto walikuwa wanaendelea kupambana na moto huo saa kadhaa baada ya mlipuko huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad