Nape: Kukamata Wahalifu wa Mtandao sio Jukumu la TCRA

 

Nape: Kukamata wahalifu wa mtandao sio jukumu la TCRA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametaja majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pale ambapo Umyanyasaji au ukatili wa kijinsia umeonekana kutendeka kwa njia ya mtandao.


Nape amesema kuwa majukumu ya TCRA kwa mujibu wa sheria sio kukamata wahalifu bali ni kuvisaidia vyombo vinavyohusika na kukamata wahalifu kisha Polisi ndio wanakwenda TCRA kupata ushahidi wa mhalifu.


Ameongeza kuwa kwa sasa changamoto iliyopo ni pale watu wengi wanapofanyiwa ubaya na kusubiri mtu mwingine achukue hatua.


“Changamoto tuliyonayo watu wengi wanafanyiwa ubaya halafu wanasubiri mtu fulani achukue hatua. Ukifanyiwa ubaya ukienda Polisi wakija kwetu tutawaunganiaha tutawapa mhalifu wao wataendelea na sheria”. Amesema Waziri Nape


Hayo yamejiri Bungeni jijini Dodoma wakati Mbunge Suma Fyandomo akichangia miswada ya Serikali ambapo alihoji TCRA wanakwama wapi pale ambapo watu wanadhalilishwa mitandaoni lakini hawachukui hatua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad