Ole Sabaya Atoa Sadaka ya Shukrani Kanisani


Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefika katika Kanisa la Ebenezer Restoration Ministry for all nations, Moshono mkoani Arusha kutoa sadaka ya shukrani.

Hii ni mara ya kwanza Sabaya kutokea hadharani kuzungumza baada ya kuachiwa na Mahakama baada ya kushinda rufaa na kesi nyingine kuachiwa kwa makubaliano ya kukiri kosa.

Sabaya amewasili kanisani hapo akiwa ameongozana na mke wake Jesca Nassari, ndugu, jamaa na marafiki na wananchi kutoka Kata ya Sambasha alikowahi kuwa diwani.

Wengine waliokuwa wanashtakiwa pamoja na Sabaya ni Sylvester Nyegu, John Odemba na Enock Mnkeni.

Aprili 5, 2023 Sabaya aliachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kwa masharti ya kutofanya kosa la jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kukiri kosa la kula njama na kuzuia utekelezaji wa haki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya kumtia hatiani Sabaya, aliyekiri kutenda makosa hayo.

Mbali na kesi hiyo, Sabaya aliachiwa katika kesi nyingine mbili zilizokuwa zikisikilizwa mkoani Arusha.

Oktoba 15, 2021, Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wanakabiliwa na kesi namba 105/2021 walitiwa hatiani baada ya mahakama kuona wamethibitika kufanya unyang'anyi wa makundi na kuhukumiwa jela miaka 30 kila mmoja, lakini walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupinga hukimu hiyo.


Mei 6, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Sedekia Kisanya, iliwafutia hatia na kuamuru waachiwe huru baada ya kushinda rufaa pia waliendelea kukaa ndani kutokana na kuwa na kesi nyingine.

Novemba 17, 2023 Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Sabaya na wenzake wawili walioachiwa huru na Mahakama hiyo.

Rufaa hiyo ya jinai namba 231/2022 ilikuwa inapinga uamuzi ulitolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha uliowaachia huru Sabaya, Nyegu na Mbura.


Baada ya Sabaya na wenzake kupangua kesi hizo kwa sasa wamebakiwa na rufaa nyingine moja namba 155/2022.

Rufaa hiyo iliyokuwa inasikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inapinga Sabaya na wenzake kuachiwa huru ambapo Februari 20, 2023 mawakili wa wajibu rufaa waliwasilisha maombi ya kufanya mapitio ya mwenendo wa rufaa hiyo.

Mbele ya Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia, alieleza mahakama kuwa walipokea maombi ya kufanya mapitio yaliyoomba mahakama hiyo ya juu ifanye mapitio ya mwenendo wa rufaa hiyo na uamuzi mdogo uliotolewa Desemba 14, 2022 hivyo kuomba rufaa hiyo isubiri kwanza
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad