Papa Francis amesema anaona kuna "unafiki" katika kukosolewa kwa uamuzi wake wa kuruhusu makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja.
Baraka za wapenzi wa jinsia moja ziliidhinishwa mwezi uliopita na hati ya Vatican iitwayo Fiducia Supplicans (Supplicating Trust), lakini ulikumbana na upinzani mkubwa katika Kanisa Katoliki, hasa kutoka kwa maaskofu wa Afrika.
Francis aliliambia jarida la Kikatoliki la Italia Credere kuwa "daima" anawakaribisha wapenzi wa jinsia moja na waliooana tena baada ya talaka kwenye sakramenti ya kuungama.