Prof Janabi Ataja Sababu Watu Kuzeeka Mapema


Profesa Janabi Muhimbili
Profesa Janabi Muhimbili


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mtindo mbaya wa maisha na kula vyakula visivyofaa, inachangia kwa kiasi kikubwa watu kuzeeka mapema.

Profesa Janabi ameyasema hayo jana Jumanne Februari 20, 2024 wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema watu hawafi kwa sababu ya uzee, lakini wanakufa kwa sababu ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na mtindo wa maisha.

“Sijui kama kuna mtu amewahi kumuona mtu amekufa kwa sababu mzee. Wengine Mungu aliwapa uhai mrefu unamuona kabisa huyu ana afya yake. Leo hii ninyi mnafahamu unaweza kukutana na mtu ana miaka 40 na mwingine miaka 30 ukadhani yule wa 30 ndiyo ana miaka 45 kumbe amezeeka mapema kutokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwamo ulaji usiofaa,” amesema Profesa Janabi.

Kwa habari zaidi kuhusu mahojiano na Profesa Janabi, usikose Jarida la Afya Februari 23, 2024 pia endelea kufuatilia Gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad