Rais Mwinyi |
Rais Mwinyi Asaini Sheria Mpya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuanza kazi kwa sheria mpya nne muhimu kutasaidia umairishaji wa shughuli za kiutendaji pamoja na kuibua kuongeza tija katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar
Rais Dkt Mwinyi ameeleza hayo wakati alipotia saini rasmi sheria nne mpya katika Viwanja vya Ikulu Mjini Unguja
Sheria hizo ni pamoja na sheria ya Mahkama ya kadhi ya mwaka 2023 ambayo imefuta sheria namba 9 ya mahakama ya kadhi ya mwaka 2017, sheria nyingine ni sheria ya kuweka masharti ya mtoaji leseni udhibiti na usimamizi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha, sheria ya Mkaguzi wa Umma ambayo imefuta sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na sheria ya uwekezaji ambayo inatajwa kuwa bora barani Afrika
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar Sharif Ali Sharif amesema sheria mpya ya uwekezaji inaenda kuongeza ukuaji wa sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya wawekezaji na kuweka vivutio mbalimbali ikiwemo kutenga eneo maalum la ardhi kwaajili ya uwekezaji visiwani Zanizbar