RASMI: Simba watangaza kumsamehe Chama, aungana na timu Kigoma

 

RASMI: Simba watangaza kumsamehe Chama, aungana na timu Kigoma
Chama Asamehewa na Simba

Klabu ya Simba SC, imetangaza kumsamehe kiungo wao mshambuliaji Clatous Chota Chama baada ya kutanguliwa na tetesi za msamaha huo.


Simba wamesema, hatua hiyo imefuatia maamuzi ya Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba ambayo ilipitia barua ya maelezo ya Chama na pia uamuzi wa Kocha Benchikha wa kumsamehe.


Hivyo Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba imeridhia kumsamehe Chama na kusitisha kumfikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Klabu ya Simba.


Chama anaungangana na kikosi cha Simba kilicho mkoani Kigoma kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC tayari kuvaana na Mashujaa FC hapo kesho Februari 3, 2024.


Taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, imeeleza kuwa itaendelea kutilia mkazo ustawi wa nidhamu kama nguzo muhimu ya kujenga timu imara, nidhamu ni moja ya tunu za Klabu ya Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad