Wakati Yanga inacheza dhidi ya Kagera Sugar nilikuwepo Bukoba, nilipata fursa ya kukaa na kuzungumza na Mkurugenzi wa Masoko na Wanachama, Ibrahim Samwel @i_sammjr .
Wakati tukizungumza akawa ananipa mpango na malengo yake ambayo ndio malengo ya klabu pia. Tukiwa tunaendelea na mazungumzo akaja mdau mmoja wa soka wa Buboka tukawa tunaendelea kupiga story baada ya muda kidogo akaja Rais wa Yanga Eng. Hersi akaungana na sisi.
Yule mdau wa soka wa pale Bukoba akajitambulisha kwa Rais wa Yanga kwamba yeye ni shabiki wa Yanga lakini anataka kujisajili na kuwa mwanachama. Eng. Hersi akamwambia Ibrahim amsaidie kumsajili.
Ibrahim akawapigia simu vijana wake wawili wakaja pale wakamsajili yule mdau, ni kitendo cha dakika chache sana yule mdau akawa kasajiliwa na kutengenezewa kadi ya kidigitali.
Akakabidhiwa kadi yake, kadi ya mke wake na watoto wawili, akalipia zoezi likakamilika palepale hakuna mambo ya kusubiri baada ya wiki mbili!
Nawapongeza Yanga kwa kubadilisha mifumo ya kizamani na kutumia teknolojia ya kisasa. Watu wanataka kujisajili kuwa wanachama lakini changamoto wanayokutana nayo ni zoezi kuchukua muda mrefu.