Mwandishi wa habari za michezo, Charles Abel amesema Tanzania lazima itengeneze mazingira bora wakati ikijiandaa kwa mashindano ya Afcon 2027.
“Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, lazima kuwe na viwanja bora bila kusahau suala la waamuzi walio bora ili kuchezesha kwa haki.
“Kingine ni miundombinu rafiki, kwani wageni watakaokuja ni wengi, hivyo lazima tujipange kutengeneza maeneo rafiki kwao,” amesema.
Amesema hayo jana Februari 14, 2024 wakati akiachangia mjadala wa Mwananchi X Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo "Tanzania imejifunza nini kupitia Afcon 2023, ikijiandaa 2027?"