Umeme Waanza Kurejea Kwa Mgao....



Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limetoa taarifa ya kurejea kwa mfumo wa umeme wa Gridi ya Taifa, huku mikoa inayohudumiwa na gridi hiyo ikiwa imeanza kupata umeme.

Leo Jumamosi Februari 3,2023 Shirika hilo lilitangaza kuwepo na hitilafu katika gridi ya Taifa na kusababisha athari katika mikoa yote inayohudumiwa na gridi hiyo.

Mikoa iliyopo kwenye Gridi ya Taifa ni Dar es Salaam, Manyara, Morogoro, Pwani, Tanga, Arusha, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora, Kigoma, Kagera, Iringa, Ruvuma, Njombe pamoja na Zanzibar.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano na uhusiano kwa umma ya shirika hilo, imesema maeneo mengi yameanza kupokea nishati hiyo wakati maeneo mengine yakiendelea kurejeshewea huduma.

"Shirika linashukuru wateja wote kwa uvumilivu wakati wa utatuzi wa hitilafu iliyojitokeza,"imesema taarifa hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad