Wabunge Wapendeza Serikali Kununua NDEGE Kwa Ajili ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikiwasilisha taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati kwa kipindi cha February 2023 hadi January 2024 Bungeni leo imependekeza Serikali kununua ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa.


Maoni hayo ya Kamati yamewasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamakati hiyo Joseph Mhagama ambapo amesema “Kamati imebaini kuwepo kwa ndege tatu zinazowahudumia Viongozi wa Kitaifa, ndege moja aina ya Gulfstream G550 inamuhudumia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nyingine Fokker F50 na Fokker 28 zinawahudumia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Kwanza na wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wengine wa Kitaifa”


“Kamati imebaini kuwa, ndege aina ya Fokker 28 ambayo ilinunuliwa mwaka 1978 ilitumika kuwahudumia Viongozi Wakuu wa Kitaifa hadi kufikia mwaka 2015, ndege hiyo imefanya kazi ya kuwahudumia Viongozi wa Kitaifa kwa miaka 39, kwa sasa ndege ya Fokker F50 inaendelea kuhudumia Viongozi Wakuu wa Kitaifa isipokuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hali hii husababisha Wakala kutekeleza jukumu la kuwahudumia Viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za Viongozi wote kwa wakati mmoja”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad