Wanaosoma Magazeti kwa Mbwembwe Kuchukuliwa hatua

 

Wanaosoma Magazeti kwa Mbwembwe Kuchukuliwa hatua

Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe huku wakiongezea baadhi ya vitu visivyotakiwa wakati wa usomaji.

Kisaka amesema hayo katika mkutano wa mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini uliofanyika Jijini Dodoma ———> “Kuna wachache wakorofikorofi wanaleta mbwembwe na kuongezea vitu pale kwenye magazeti kwahiyo nafikiri hao pia watamulikwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria, ni wachache sana”

“Kanuni za matumizi ya lugha zipo kama unaongea kiingereza ongea kiingereza kama unaongea kiswahili ongea kiswahili, hivi kuna haja ya kukiita kipindi Good Morning?, tumesilisika kabisa kuita vipindi vyetu kwa lugha ya kiswahili”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad