Wasanii wa Lebo Waliotelekezwa na Lebo zao Kwa Kukaa Muda Mrefu Bila Kazi

Wasanii wa Lebo Waliotelekezwa na Lebo zao Kwa Kukaa Muda Mrefu Bila Kazi


Lebo za muziki zina jukumu muhimu katika maisha ya wasanii na muziki wao. Zinatoa fursa za kipekee za kukuza talanta zao na kufikia hadhira kubwa zaidi.

Mbali na hilo, lebo hizi huchangia sana katika mafanikio ya wasanii kwa kusimamia masuala ya kifedha na kisheria, kutoa rasilimali za kurekodi na kutengeneza muziki, pamoja na kusaidia katika masuala ya masoko na uendelezaji wa kazi zao.

Hapa Tanzania kuna baadhi ya wasanii ambao waliwahi kutambulishwa kwenye lebo na kuachia kazi kadhaa lakini hivi sasa ni kama hawapo tena kwenye industry kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kuachia kazi mpya. Miongoni mwao ni pamoja na;

1. The Great Eddy - Alitambulishwa mwaka 2021 na The Industry chini ya @aikanavykenzo na @nahreel kisha kuachia project yake ya kwanza SMALL BAD WOLF ikiwa na ngoma 6 mwezi Aprili. Hata hivyo, licha ya kipaji chake, @thegreat.eddy amekuwa kimya kwa kiasi kikubwa tangu wakati huo.

2. Queen Darleen - Tangu mwaka 2022, Dizzo amejitenga na maisha ya muziki na mitandao ya kijamii. Msanii huyo wa WCB Wasafi anatazamiwa huenda mwaka huu akarejea upya baada ya mapumziko hayo, yaliyozua hofu kuhusu msanii huyo na maisha ya lebo yake.

3. Mulla - Mwanzilishi wa HIGH TABLE SOUND, @barnabaclassic, alitoka kwenye vyombo vya habari mwaka 2019 na kufichua nia yake ya kusaidia vijana. Miongoni mwa walioshikwa mkono na Mopao alikuwa @mullaobo, ambaye amefanya kazi kadhaa lakini hajapata mwendelezo ulio bora.

4. Mac Voice - Kipaji kingine kutoka @nextlevelmusic_tz, msanii aliyetambulishwa na @rayvanny miaka miwili iliyopita na kuachia EP, MY VOICE iliyokuwa na hits kama Tamu, Nenda na zingine.

Baada ya kukaa kimya miezi sita @macvoice_tz anaijiandaa kurejea na kazi mpya NIAMBIE aliyo-tease wiki mbili zilizopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad