Yanga Viherehere Sana, Point 40 za Kuongeza Ligi Waanza Kufikiria Paredi la Ubingwa



Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe akizungumza na SportsXtra ameweka wazi takwimu zao na mwisho amehitimisha kwa kusema takwimu zinawapa nguvu ya kuafikiria route ya parade la ubingwa akiwa na maana msimu huu watabeba tena.

“Kimsingi ligi ina mechi 30, ukicheza mechi 15 maana yake umefikisha nusu na ndio maana inaitwa mzunguko wa kwanza,kwenye hizi mechi 15 tumekusanya pts 40, msimu uliopita tulikusanya pts 38 maana yake msimu huu tumeongeza pts 2 mbili zaidi , kwenye pts 45 tumedondosha tano “

“Magoli ya kufunga ,msimu huu tumefunga magoli 36 ,msimu uliopita tulifunga magoli 28 ,ukipiga hesabu magoli 8 yameongezeka”

“Msimu uliopita tulipata ushindi wa magoli 5 kwenye mechi moja , msimu huu kwenye Ligi tumefunga magoli 5 kwenye mechi 3”

“Kwa takwimu hizi kama kiongozi inakupa hamu na kuanza kufikiria njia (route) za parade”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad