Zawadi za Boxer Kwa Wachezaji SIMBA ziliishia Wapi? Je ni Sababu ya Simba Kutokuwa Bora Kama Zamani?

 

Zawadi za Boxer Kwa Wachezaji SIMBA ziliishia Wapi? Je ni Sababu ya Simba Kutokuwa Bora Kama Zamani?


Wanaomkwamisha Tajiri wapo /Wapi..?


Mwaka 2019 Tajiri MO DEWJI aliamua kuingia mfukoni na kutoa zawadi ya MO BOXER & RICE COOKER kwa Benchi la Ufundi la Simba na Wachezaji wote wa simba baada tuu ya kufanya vizuri kwa kutwaa Ubingwa wa ligi kuu na Kufika robo fainali Klabu bingwa Afrika.


Moja ya Jambo ambalo liliifanya Simba iendelee kuwa bora ni kutokana na Tajiri kufungua pochi yake na kutoa bonasi nyingi kwa Timu kila inapofanya vizuri.


Zawadi za Pikipiki na & Rice Cooker inawezekana zilichukulia ni za kawaida lakini imani yangu ziliacha alama kubwa sana kwa wachezaji waliokuwepo Simba mwaka 2019.


Moja ya Jambo ambalo linaifanya Simba ya Sasa isiwe bora sana imani yangu ni Kupunguzwa kwa Bonasi lukuki ambazo wachezaji walikuwa wanapata, Hivi Yupo aliyejiuliza kuwa kama Tajiri asingevurugwa timu ingekuwa kwenye Ubora upi.


Mara kadhaa amekua akisema kuna watu wana mkwamisha, mabadiliko ya Katiba natumaini yataenda kurejesha Furaha kwa wanasimba na Tajiri mwenyewe.

By Kijiwe Nongwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad