Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha, kukatisha ameamua masomo yake na kurejea nchini kuanza mikakati ya kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa Benchikha aliondoka nchini kuelekea Algeria siku chache zilizopita kwa ajili ya kuhudhuria kozi ya juu ya ukocha, lakini baada ya kutangazwa Droo ya Robo Fainali ameamua kukatisha kozi hiyo na kurejea nchini.
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo amesema kuwa kocha huyo anatarajiwa kurejea nchini siku yoyote kuanzia leo Alhamis (Machi 14) na tayari ametoa maombi kwa uongozi kuipeleka timu hiyo Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi katika kipindi ambacho ligi itasimama kupisha mechi za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’.