Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Rais Samia amemteua pia Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Mtanda ambapo kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.