BASHE: Waambieni Wamarekani Tuna Michele na Maharage ya Kutosha Tanzania



Baada ya kuibuka kwa mjadala katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania, baada ya serikali ya Marekani kwa ushirikiano na jumuiya za kimataifa kutoa msaada wa chakula kwa shule zilizopo mjini Dodoma. Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema kuwa waagizaji hawakupaswa kuleta msaada huo wa chakula kwani Tanzania ina chakula cha kutosha ikiwemo hazina ya kutosha ya mchele na maharage.

"Tumewaambia ile NGO, waambieni Wamarekani hivi, mchele upo maharagwe yapo nchi hii, zile fedha wanazotumia kuwapa wakulima wa Marekani wawape Watanzania. Tununue mchele kutoka Tanzania, maharagwe kutoka Tanzania, halafu hivyo virutubisho mnavyotaka kuweka tuwekee hapahapa wote tunaona''.

Bashe aliongeza pia kuna changamoto ya kutokua na ushirikishwaji katika miradi, na miradi mingi hujiendesha kivyake.

Ruka Twitter ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Kuhusu mradi
Kwa mujibu wa mtandao wa jumuiya za kimataifa, USDA ilikabidhi Global Communities mradi wa miaka mitano unaoitwa, Pamoja Tuwalishe. Jumuiya za Kimataifa zitatoa usaidizi wa kiufundi na kuambatana na taasisi muhimu za kiserikali na zisizo za kiserikali ili kuendesha lishe endelevu, jumuishi shuleni katika mikoa ya Mara na Dodoma na kusaidia kuanzishwa kwa Mwongozo mpya wa Serikali ya Tanzania wa utoaji wa chakula katika shule.

Katika kipindi chote cha mradi, Pamoja Tuwalishe itatoa tani 3,830 (MT) za bidhaa zilizotolewa na Marekani - mchele, maharagwe, mafuta ya kula - pamoja na fedha zinazotolewa na USDA ili kununua 1,565 MT ya bidhaa zinazolimwa na kununuliwa kama mahindi, maharagwe. , mafuta ya alizeti. Bidhaa za chakula zinazotolewa na mradi, pamoja na chakula kinachochangwa na shule, jamii na Serikali ya Tanzania, vitatoa chakula shuleni kwa zaidi ya wanafunzi 300,000 wa shule za awali na msingi katika shule 351 katika wilaya tisa za mikoa ya Mara na Dodoma.

Chanzo cha picha, US Embassy Tanzania

w
Maelezo ya picha, Magunia ya maharage kutoka Marekani.
Msaada huo unashirikisha mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani

Kulingana na Marekani mpango huo unaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni.

Hatahivyo hatua hiyo haikupokelewa vyema na watumiaji wa mitandao nchi humo waliohoji iwapo taifa hilo linahitaji msaada wa chakula

Ruka Twitter ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Elias G balimponya katika mtandao wake wa X alihoji: Hivi Tanzania tunahitaji msaa wa chakula kweli? Aliongezea: Chakula??? MAHARAGWE, MCHELE, MAFUTA YA ALIZETI??

Alisema: Ndugu zangu Marekani njooni tushirikiane katika mambo mengine muhimu ya kuinua uchumi. Tanzania kusaidiwa chakula HAPANA . Natamani kumfahamu kiongozi wangu aliyeomba msaada wa CHAKULA. Jamaa huyo badala yake aliitaka Marekani kutoa misaada kama hiyo kwa taifa la Sudan

Kwa upande mwengine mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina CAT POWER alishutumu hatua hiyo akitaka waziri aliyepokea msaada huo kufutwa kazi mara moja..

Alisema kwamba Tanzania ni mlimaji mkubwa wa mchelele wa kutosha hadi unakosa soko. Alihoji ni vipi watumie mchele wenye virutubishi kutoka Marekani?.

Mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina Lings, aliuliza maswali kadhaa. Je tumefika huku? Ni kweli tuliomba hiki chakula? Je tunakufa njaa? Hatuwezi kulisha watoto wetu? Mchele? Kweli Mchele? Kwanini wasipeleke nchi zenye njaa?

Aliendelea kusema: Nina hakika kwamba hatukuomba wala hatuhitaji, Wanatupa michele?

Mwengine kwa jina Yoab Mwana wa Seruya alisema: Tunashukuru lakini, HAPANA hatuhitaji huu mchele. Alisema Mchele wetu wa Mbeya upo wa kutosha sana. Alitaka msaada huo wa chakula kupelekwa katika kambi za wakimbizii huko Kigoma. Aliongezea: Au pelekeni Sudan Kusini .Sisi Hatuutaki. Taifa letu linajitosheleza kwa Chakula alihitimisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad