Kocha wa Klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha, ameeleza kuwa kinachomgharimu ndani ya timu hiyo ni kukosa namba kubwa ya wachezaji wa daraja la juu.
Akizungumza baada ya kupoteza dhidi ya Al Ahly Benchikha amesema ubora ndio ulioamua matokeo katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.
"Unapopata nafasi zaidi ya sita kwenye box la mpinzani unahitaji wachezaji wenye uwezo wa kuzitumia nafasi hizo
"Mfano wenzetu Al Ahly wana Modeste, Kahraba, ambao wote hawa wanaweza kuzitumia nafasi hizo" amesema Benchikha baada ya mchezo.
Ameongeza kuwa ufinyu wa wachezaji wenye ubora kikosini unamgharimu ndio maana alipofanya mabadiliko bado hakupata kitu ambacho alikitamani tofauti na ikivyokuwa kwa wapinzani wake.
Una maoni, tuandikie