“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madal hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao”
“Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara” imeeleza taarifa hiyo ya bunge