Daladala na Abiria Wasusia Kituo Kipya Cha Abiria Mwenge

Daladala na Abiria Wasusia Kituo Kipya Cha Abiria Mwenge



Baadhi ya abiria wa wanaoanzia safari mituo kipya cha Mwenge, wamelalamikia kukaa muda mrefu bila kupata usafiri na kulazimu kwenda kutuo cha Makumbusho.

Times Digital ilifika na kushuhudia idadi ndogo ya daladala zikiingia na kutoka, huku ikipita zaidi ya nusu saa bila gari lolote kuingia.

Kwa siku tofauti Times Digital, iliongea na baadhi ya abiria wa Mbagala, walisema kuwa hupita hata dakika 60 bila gari kufika, hivyo kuiomba LATRA kuongezea ruti mpya za kuanzia hapo.

Upande wake Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Dar es Salaam, Rahimu Kondo amesema uchache wa magari kituoni hutokana na waombaji wa ruti hiyo kutochangamkia fursa ya ruti na baadhi abiria kuanzia kituo Mpakani na vituo vingine.

Aidha, amewataka wananchi kutumia kituo hicho kwani kina mindombinu bora na sahihi kwa ajili yao ikiwemo sehemu salama ya kusubria gari huku ukiwa umejikinga na mvua ,Jua na kupumzika.

Hata hivyo, amewaomba wamiliki wa magari kuendelea kuongeza maombi ya ruti kuanzia hapo Mwenge kwani nafasi bado zipo za kutosha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad