Dereva wa Mwendokasi Adaiwa Kuwapitiliza vituo abiria kwa hasira

 

Dereva wa Mwendokasi Adaiwa Kuwapitiliza vituo abiria kwa hasira

Dereva wa Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) ambaye jina lake halijafahamika, akiendesha kutoka kituo cha Gerezani kwenda Kimara, amedaiwa kutosimama kwenye vituo vingi vya njiani baada ya kurushiana maneno na Abiria ambao walilalamikia uendeshaji wake.


Abiria mmoja amedai licha ya Basi kujaa, Dereva aliendelea kupakia abiria ambapo walilalamika kuwa anawaumiza kwa kufungua na kufunga milango, hali iliyoibua ubishani.


Baada ya kutoka Kituo cha Magomeni Dereva hakusimama, akawapeleka abiria wote Kituo cha Kimara Mwisho.


Anadai walipofika Kimara, Dereva alishuka na kuondoka na baada ya mvutano wa muda mrefu, Dereva mwingine akaamua kuchukua basi husika na kuwarejesha wale waliopitilizwa vituo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad