Diamond Platnumz na Harmonize Kutoa Remix ya Wimbo wa Kwangaru, Tajiri Aweka Pesa Mezani



Hizi ni kutoka ndani ya vikosi kazi vyote. Kwa Diamond na Team ya WCB yake pamoja na Harmonize na Team ya Konde Gang yake. Balaa la pini la Taifa la Kwangwaru linajirudia kwa mara nyingine tena.

Ni katika ngoma mpya kati ya Mondi na Konde, waliopanga pamoja kuitengeneza 'suuni' na kuratibiwa na Mondi, Konde mwenyewe pamoja na kampuni moja kubwa.

Maneno yaliyosikika kati yao Ikulu jana jioni, wakiambiana suala la kupigiana simu, kumbe ile ilikuwa zuga tu bali ni 'dili' la ngoma ya pamoja, ambalo linasimamiwa na kampuni moja kubwa ya (eti ni kampuni ya simu).

Kwa sasa siyo rasmi, lakini habari za 'aminifu' zenye upako, zimemwagwa kwenye fito za meza za Times Digital, mchana huu zikidai Dimaond na Harmonize wamesaini mamilioni ya dola kwa ajili ya 'projekti' hiyo ya pamoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad