Fei Toto Awaomba Msamaha Yanga Baada ya Kuwafunga

 

Fei Toto Awaomba Msamaha Yanga Baada ya Kuwafunga

Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa leo usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku kiungo Feisal Salum ' Fei Toto' akifunga na kuomba msamaha.


Fei Toto aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Yanga, amewafunga waajiri wake wa zamani lililokuwa bao la pili na la ushindi kwa Azam dakika ya 52 ya mchezo.


Baada ya kufunga Fei Toto alishangilia kidogo, k isha kuonyesha ishara ya kuomba msamaha kwa mashabiki wa Yanga ambao wakati anaondoka alikuwa kwenye mgogoro wa kimkataba na timu hiyo.


Bao la Fei Toto limekuwa la 13 kwa msimu huu na kulingana na Stephanie Aziz Ki wa Yanga.


MCHEZO ULIVYOKUWA


Timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa kushitukiza huku utulivu ukitawala kwa pande zote mbili kwenye kujilinda zaidi.


Dakika ya 10, Yanga iliandika bao la kuongoza kupitia kwa Mzize aliyefunga baada ya kupikea pasi safi ya Aziz Ki ikiwa ni asisti ya saba kwa Mburkina Faso huyo msimu huu kwenye ligi .


Azam ilisawazisha bao hilo dakika ya 19 kupitia kwa kiungo Djibril Sylla aliyefunga baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuondoa mpira kwenye eneo Lao la hatari.


Staa wa Yanga, Pacome Zouzoua alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 31 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Straika Joseph Guede.


Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya mabao 1-1, na kipindi cha pili kilivyorejea timu zote mbilizianza kwa utulivu na kucheza kwa Kasi ya wastani.


Dakika ya 52, Fei Toto aliifungia Azam bao la pili kwa shuti baada ya kukutana na mpira akiwa katika boksi la hatari la Yanga.


Yanga ilifanya mabadiliko mawili dakika ya 58 kwa kuwatoa Nickson Kibabage na Maxi Nzengeli na nafasi zao kuchukuliwa na Kennedy Musonda na Joyce Lomalisa.


Dakika ya 80 Yanga ilifanya mabadiliko engine mawili kwa kuwatoa Koassi Yao na Mzize na kuingia Augustine Okrah na Bakari Mwamnyeto na Azam ikajibu mapigo kwa kumuingiza Idi Seleman. 'Nado' aliyechukua nafasi ya Abdallah Seleman 'Sopu'.


Dakika ya 86 Azam ilifanya mabadiliko mengine mawili kwa kuwatoa Paschal Msindo na Sylla na kuingia Cheikhe Sidibe na Ayoub Lyanga ambao waliimarisha timu na kulinda ushindi.


Ushindi huo umeifanya Azam kufikisha alama 47 baada ya mechi 21 na kukaa nafasi ya pili ikiishusha Simba yenye pointi 45 kwa mechi 19 nafasi ya tatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad