Gamond Afunguka "Mamelod Nawajua Niliwafundisha Hadi Wakachukua Ubingwa"



Mamelodi Sundowns ni timu ambayo nimewahi kuifundisha zamani, nilifanikiwa kushinda ubingwa Ligi ya Afrika Kusini mwaka 2006 nikiwa kocha wa Mamelodi. Nina furahi kucheza nao katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni timu kubwa na inacheza aina ya soka linalofanana na sisi, kwa upande wa Yanga huu ni wakati mzuri kushindana na timu kubwa na kama tunahitaji kuwa miongoni mwa klabu kubwa Afrika ni lazima tushindane.

Mamelodi ni aina ya timu kama Al Ahly, kila msimu wanataka kucheza hatua ya Fainali na kushinda ubingwa wa Afrika kwa sababu ni klabu kubwa. Kama utalinganisha bajeti ya Mamelodi na sisi bado tupo mbali sana, mara ya mwisho wamesajili mchezaji kwa dola [USD] milioni nne wakati sisi tulimsajili Okrah akiwa mcheaji huru.

Hiyo ndio tofauti na watu wanapaswa kuelewa lakini hiyo haijalishi, mwamuzi akipiliza filimbi uwanjani ni 11 dhidi ya 11. Tunapaswa kupambana na kupigana zaidi ya Mamelodi.

Kabla hatujacheza dhidi ya Al Ahly nilisema tofauti yetu ni uzoefu wa kucheza mechi kubwa. Tulifanya makosa hapa na tulifanya makosa kwao [Misri] lakini mara zote mchezo wa soka ni mchezo wa makosa.

Kwa sasa Yanga imeimarika, imeshinda Ligi mara mbili mfululizo, imeshinda kombe la FA mara mbili mfululizo, imecheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, imecheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kufuzu Robo Fainali mbele ya CR Belouizdad.

- Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad