Hali ya Uchumi Singida Fountain Imeyumba, Bruno Gomez Avunja Mkataba



Mchezaji wa imataifa wa Brazil Bruno Gomes kupitia ukurasa wake wa Instagram, ametangaza kusitisha mkataba wake wake na Singida Fountain Gate FC baada ya makubaliano ya pande mbili.

Bruno ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Napenda kuwajulisha kuwa, kumekuwa na uvunjwaji wa mkataba kwa upande mmoja kutoka kw klabu, na kwa bahati mbaya hii imesababisha kumalizika kwa uhusiano wangu na klabu hiyo.

“Uamuzi huu hauliwa rahisi, lakini ulifanyika kwa nia ya kuhakikisha tunaweza kuendelea mbele kwa njia ambayo ni chanya na yenye ujenzi kwa wote.”

Kuondoka kwa kiungo huyo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate FC kunaifanya klabu hiyo kuondokewa na wachezaji wengi muhimu baada ya wale waliojiunga na Ihefu wakati wa dirisha dogo la usajili.

Taarifa nilizonazo ni kwamba viongozi wameshindwa kumudu kiwango cha pesa walichokubaliana awali kumlipa kiungo huyo ,hiyo imetosha kuwa sababu ya Bruno kuwabwaga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad